Spotify Yazizima! Drake Afikisha Rekodi Isiyowahi Kutokea

Rapper maarufu kutoka Canada Drake ameendelea kuandika historia katika muziki wa HipHop baada ya kuwa msanii wa kwanza wa HipHop duniani kufikisha wasikilizaji bilioni 4 kwenye jukwaa la Spotify.

Rekodi hiyo inaonesha ukubwa wa ushawishi wa Drake katika muziki wa kimataifa pamoja na nguvu ya mashabiki wake waliopo kila kona ya dunia kwa zaidi ya muongo mmoja Drake ameendelea kutawala chati mbalimbali, kuvunja rekodi za streaming na kuachia nyimbo zilizodumu kwa muda mrefu sokoni.

Miongoni mwa nyimbo zilizochangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo ni “One Dance”, wimbo uliotoka mwaka 2016 kupitia albamu ya Views. Licha ya kupita zaidi ya miaka tisa tangu kutolewa kwake wimbo huo bado unaendelea kusikilizwa kwa wingi hadi leo.

Wimbo wa One Dance pia unambeba msanii kutoka Nigeria, Wizkid, ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa waandishi wa wimbo huo. Ushirikiano huo uliifanya One Dance kuwa daraja muhimu kati ya HipHop, Dancehall na Afrobeats, na kuipa muziki wa Afrobeats nafasi kubwa zaidi katika soko la kimataifa.

Kupitia wimbo huo Drake na Wizkid waliweka alama isiyofutika katika historia ya muziki wa dunia. One Dance uliwahi kushika nafasi ya kwanza katika chati mbalimbali ikiwemo Billboard Hot 100, na kubaki kuwa miongoni mwa nyimbo zinazostreamiwa zaidi muda wote.

Hata hivyo kwa kufikisha wasikilizaji bilioni 4 Spotify rekodi ya Drake si ushindi wake binafsi pekee, bali pia ni ushahidi wa ukuaji na ushawishi wa muziki wa HipHop na Afrobeats katika kuvuka mipaka ya kijiografia na kufikia hadhira ya dunia nzima.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii