Niffer Athibitisha Kuachana na OG, Aomba Kuheshimiwa

Mfanyabiashara maarufu anayefahamika kwa jina la Niffer amethibitisha rasmi kuvunjika kwa mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake OG Phone and Accessories akieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa utulivu heshima na bila chuki wala maumivu.

Hata hivyo kupitia taarifa aliyoiweka wazi kwa umma Niffer amesema amechukua muda wa kutosha kutafakari kabla ya kuzungumza, akibainisha kuwa kwa kuwa yeye ndiye aliyeyaweka mahusiano yao hadharani tangu mwanzo, ameona ni vyema pia kuwa muwazi kuhusu hatua aliyofikia sasa.

Akitumia methali ya “Kitanda usicholalia hujui kunguni wake,” Niffer ameashiria kuwa si kila kinachoonekana kwa macho ya watu ndicho uhalisia wa mambo yaliyokuwa yakitokea ndani ya mahusiano yao. Ameongeza kuwa kutamani kuona mabadiliko chanya kwa mtu hakuhakikishi kuwa mabadiliko hayo yatatokea, hata kama jitihada zimefanyika kwa kiwango kikubwa.

Niffer ameeleza kuwa kwa sasa yupo katika kipindi cha mpito katika maisha yake, akikitaja kuwa ni kipindi kigumu chenye mabadiliko mengi. Hata hivyo, ameonesha imani yake kwa Mwenyezi Mungu, akisema licha ya kuona mambo aliyoyathamini yakiondoka katika maisha yake, anaamini yote yanatokea kwa kheri, akisisitiza kwa neno “Alhamdulillah.”

Ameongeza kuwa kuacha nyuma mambo uliyozoea si jambo rahisi lakini pale muda unapofika uamuzi huo huwa wa lazima. Ameweka wazi kuwa hana kinyongo wala lawama kwa upande wowote akiamini kuwa kila hatua anayopitia ni sehemu ya mpango wa Mungu katika maisha yake.

Katika hitimisho la ujumbe wake Niffer amesisitiza kuwa hataki tena kuzungumzia wala kuulizwa chochote kuhusiana na aliyekuwa mpenzi wake OG Phone and Accessories iwe kwa mtazamo chanya au hasi. Amewaomba watu wanaompenda kuheshimu uamuzi wake na kutambua kuwa mahusiano hayo hayakufikia mwisho mwema kama ilivyotarajiwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii