Wiz Khalifa Ahukumiwa Jela Romania kwa Kosa la Dawa za Kulevya

Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Wiz Khalifa, amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na Mahakama ya Romania kwa kosa la kuvuta bangi hadharani wakati wa onyesho la muziki.

Rapa huyo, ambaye jina lake halisi ni Thomaz Cameron Jibril, alikiri kuvuta bangi akiwa jukwaani wakati wa tamasha la Beach, Please! lililofanyika mwaka 2024 katika mji wa Costinești, nchini Romania.

Mahakama ilitoa hukumu hiyo akiwa hayupo, huku ikibainika kuwa Wiz Khalifa alikuwa na zaidi ya gramu 18 za bangi, kinyume na sheria za nchi hiyo. Polisi walisema sehemu ya bangi hiyo ilitumika moja kwa moja jukwaani mbele ya mashabiki.

Hadi sasa haijafahamika kama rapa huyo yupo Romania, kwani alionekana mara ya mwisho Jumanne akitumbuiza nchini Marekani, akishirikiana na rapa Gunna huko California.

Baada ya tukio hilo, Wiz Khalifa aliandika ujumbe kwenye mtandao wa X, akiomba radhi na kusisitiza kuwa hakukusudia kuidharau au kukiuka heshima ya Romania.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii