Mtandao wa kijamii wa TikTok umechukua hatua muhimu ya kibiashara kwa kufikia makubaliano ya kuanzisha ubia na kampuni za Marekani, hatua inayolenga kutatua changamoto za kisheria na kiusalama zilizokuwa zikiukabili mtandao huo nchini humo.
Kupitia ushirikiano kati ya kampuni mama ya TikTok, ByteDance ya China, pamoja na kampuni za Marekani za Oracle na Silver Lake, na mfuko wa uwekezaji wa Falme za Kiarabu (MGX), umeundwa ubia mpya utakaofahamika kama TikTok USDS Joint Venture.
Aidha Kampuni hiyo mpya itaendeshwa chini ya usimamizi na udhibiti mkubwa wa wawekezaji wa Marekani, huku ikipewa jukumu la kusimamia usalama wa data za watumiaji pamoja na masuala yanayohusiana na usalama wa taifa la Marekani.
Hata hivyo TikTok imesema kuwa kwa sasa ina zaidi ya watumiaji milioni 170 nchini Marekani, idadi inayofanya soko hilo kuwa moja ya masoko yake makubwa zaidi duniani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime