Kura yapigwa kufupisha kifungo cha miaka 27 gerezani alichozabwa Rais
WABUNGE nchini Brazil mnamo Jumatano walipiga kura kufupisha kifungo ambacho Rais Jair Bolsonaro aliangushiwa kutoka miaka 27 hadi miaka miwili.
Mswada walioupitisha kufupisha adhabu hiyo, hata hivyo huenda ukapata pingamizi kutoka mwa maseneta, Mahakama ya Juu na Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva.
Kulikuwa na fujo bungeni wakati wa kupiga kura kwa mswada huo mnamo Jumatano jioni.
Mwezi uliopita Bolsonaro alianza kutumikia kifungo chake baada ya kupatikana na hatia ya kupanga njama ya kupindua utawala wa Lula baada ya kupoteza uchaguzi wa 2022.
Wabunge 291 waliunga mkono mswada wa kumfaa Bolsonaro huku 148 wakiupinga.
Mswada huo unalenga pia kupunguza kifungo kwa raia ambao walinyakwa wakati ambapo wafuasi wa Bolsonaro walivamia ikulu, Mahakama ya Juu na Bunge mnamo Januari 2023.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada Seneta Flavio Bolsonaro, mwanawe mkubwa wa kiume wa Bolsonaro kutangaza kuwa anapanga kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbunge aliyewasilisha mswada huo Paulinho da Forca alikataa vishawishi vya wabunge kuwa Bolsonaro na wote walioshiriki maandamano hayo waachiliwe huru.
“Hakuna cha kuachiliwa huru kwa sababu tumezungumza na wadau wote na njia pekee ya kuhakikisha amani ni kupunguza vifungo vyao,” akasema Paulinho.
Zaidi ya watu 2,000 walinyakwa baada ya maandamano hayo jijini Brasilia ambayo yalilinganishwa na yaliyotokea Amerika Januari 2021 baada ya Donald Trump kushinda urais.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii