Wiz Khalifa Ahukumiwa Jela Romania kwa Kosa la Dawa za Kulevya

Staa mkubwa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Wiz Khalifa amehukumiwa na Mahakama ya Romania kifungo cha miezi tisa jela kwa kosa la kuvuta bangi jukwaani akiwa anafanya shoo nchini humo.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Thomaz Cameron Jibril, alikiri kuvuta bangi wakati wa onyesho lake katika tamasha la Beach, Please! lililofanyika mwaka 2024 katika Mji wa Costinești, Romania.

Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani, na haijulikani iwapo Wiz Khalifa yupo nchini Romania, kwani mara ya mwisho alionekana Jumanne akiwa anatumbuiza pamoja na Gunna, California nchini Marekani.

Maafisa wa polisi wa Romania walisema alikuwa na zaidi ya gramu 18 za bangi na alitumia kiasi kingine akiwa jukwaani, jambo ambalo ni kinyume na sheria za Romania.

Wiz Khalifa alisema katika chapisho lake kwenye mtandao wa X siku moja baada ya tukio hilo kuwa hakukusudia kuikosea heshima nchi hiyo na kuomba radhi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii