Msanii wa Bongo Flava nchiniTanzania@rayvanny , ameendelea kuweka rekodi na kuthibitisha ukubwa wake kimataifa baada ya wimbo wake “Oh Mama Tetema” kupata tuzo ya 8× Gold nchini India, ikiwa ni mauzo ya muziki na streams.
Mafanikio haya yanaifanya “Oh Mama Tetema” kuwa moja ya nyimbo za Rayvanny zilizofanya vizuri zaidi duniani huku ikivunja rekodi ya awali ya “Tetema” iliyopata Gold moja nchini Colombia.
Rayvanny ameahidi kuendelea kusukuma muziki wake mbele kwa kusema kuwa atavunja rekodi zake mwenyewe siku zijazo.
Aidha Rayvanny sasa anazidi kukita mizizi kama mmoja ya Wasanii wakubwa barani Afrika na duniani, huku mchango wake katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava ukizidi kutambulika kimataifa.
Hata hivyo Tuzo ya Gold kikawaida inahesabiwa kulingana na mchanganyiko wa mauzo ya muziki na streams. Hi ikimaanisha wimbo wa #OhMamaTetema umepata mafanikio makubwa ya wimbo katika mauzo na usikilizwaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, #Rayvanny amejivunia mafanikio hayo huku akisema:
“Hakuna kenge wala mjusi wa kugusa hizi mambo nchi hii. Naweka rekodi ambazo nakuja kuzivunja tena mimi mwenyewe. Tetema ya Colombia ilipiga Gold moja, hii imepiga mara nane.”
Wimbo “Oh Mama Tetema” ni kolabo ya kimataifa inayowakutanisha Rayvanny, Nora Fatehi, Shreya Ghoshal, Vishal Mishra, Sanjoy na Bhushan K, na umeendelea kupaa katika majukwaa ya kimataifa kutokana na ushirikiano huo wa Afrika na India.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime