Rais wa Zamani wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol Apatikana na Hatia

Rais wa zamani wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, ambaye aliondolewa madarakani, ametiwa hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kughushi nyaraka, kuhusiana na jaribio lake lililoshindikana la kutangaza sheria ya kijeshi mwaka 2024.

Mahakama ya Seoul inaendelea kuchunguza iwapo Yoon pia alihujumu utekelezaji wa haki kwa kujaribu kukwepa kukamatwa. Katika kesi hiyo, waendesha mashtaka wameiomba Mahakama imhukumu kifungo cha miaka 10 jela.

Hukumu hiyo ni ya kwanza kati ya kesi nne zinazomkabili, zote zikihusishwa na amri yake ya ghafla ya sheria ya kijeshi.

Ingawa hatua hiyo ilidumu kwa muda mfupi, iliisukuma nchi kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa, ukishuhudia maandamano ya wananchi na wabunge kukimbilia bungeni ili kufuta uamuzi huo.

Uamuzi wa Mahakama uliotolewa Ijumaa unatazamwa kama ishara ya mwelekeo wa kesi nyingine zinazomkabili Yoon, zikiwemo tuhuma za ukiukaji wa sheria za kampeni na matumizi mabaya ya mamlaka.

 #10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii