Spika wa Bunge la India Mheshimiwa Shri Om Birla amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu katika ofisi za Bunge la India jijini New Delhi.
Mkutano huo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 28 wa Maspika na Wenyeviti wa Mabunge wa Jumuiya ya Madola unaoendelea nchini India.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya Tanzania na India, kubadilishana uzoefu katika utendaji wa mabunge, pamoja na kukuza diplomasia ya bunge kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Ziara hiyo ya Spika Zungu ni sehemu ya jitihada za Tanzania kuendeleza mahusiano ya kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge na ushirikiano wa maendeleo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime