Watu 169 Wauawa Kaskazini mwa Sudan Kusini

Watu 169, wakiwemo maafisa wakuu wa Sudan Kusini, wameuawa kufuatia shambulio lililotekelezwa na watu wasiojulikana katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumapili.

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Ruweng, James Monyluak Mijok, washambuliaji hao wanadaiwa kutoka jimbo jirani la Unity na kuwa na uhusiano na Sudan People's Liberation Army-In Opposition (SPLA-IO).

Hata hivyo, SPLA-IO imekanusha kuhusika na shambulio hilo, ikiishutumu serikali ya jimbo la Unity kwa kuingiza siasa katika ghasia hizo.

Umoja wa Mataifa umeendelea kuonya kuwa Sudan Kusini iko katika hatari ya kurejea katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe iwapo hatua za haraka za kisiasa na kiusalama hazitachukuliwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii