UN: Zaidi ya wahamiaji 7,600 walikufa njiani mwaka 2025

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limebainisha kwamba zaidi ya wahamiaji 7, 600 wasio na vibali walifariki dunia au walipotea kote duniani wakiwa njiani mwaka uliopita.

Ripoti iliyotolewa na shirika hilo Alhamisi imeeleza kuwa idadi hiyo ni ya vifo vilivyoripotiwa rasmi. Idadi kamili inaaminika kuwa kubwa zaidi lakini haiwezi kufuatiliwa kutokana na uhaba mkubwa wa fedha unaolikabili shirika hilo.

Mwaka 2024 IOM iliripoti vifo vya wahamiaji 9,200 idadi ambayo ni kubwa zaidi tangu shirika hilo lilipoanza kufanya ufuatiliaji mwaka 2024.Bahari ya Mediterania hatari zaidi kwa wahamiaji waio na vibali

Hata hivyo kulingana na ripoti hiyo, Bahari ya Mediterania ndiyo njia hatari zaidi ya uhamiaji. Kufikia Februari 24 mwaka huu, tayari mamlaka zimehifadhi kumbukumbu ya vifo 606 kwa mwaka huu pekee ongezeko ambalo ni kubwa ikilinganishwa nwa vifo 285 vilivyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2025.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii