Wawili Wafariki na wengine kujeruhiwa ajali Morogoro

Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha gari dogo aina ya Subaru lenye namba za usajili T 743 EKD kugongana na lori lililokuwa limebeba shehena ya mahindi katika barabara kuu ya Morogoro–Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea Aprili 9, 2026 eneo la Moseka, Kata ya Mkambarani, Wilaya ya Morogoro .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Andrew Kantimbo, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo, ambaye alijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari ya kutosha, hali iliyosababisha kugongana uso kwa uso na lori hilo.

Aidha miongoni mwa waliofariki ni mtumishi mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, huku majeruhi wawili wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo jeshi la Polisi limewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, hasa wakati wa kupishana na magari mengine kwenye barabara kuu, ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii