Tetemeko la ardhi lawauwa watu wanane nchini Afghanistan

Watu wanane wa familia moja wameuawa usiku wa kuamkia leo katika tetemeko la ardhi lililokumba eneo la Gosfand Dara mkoani Kabul, nchini Afghanistan.

Hayo yamesemwa leo na wizara ya afya nchini humo na msemaji wa wizara hiyo ya afya Sharafat Zaman, amesema mtoto wa umri wa takriban miaka miwili ndiye manusura wa pekee wa familia hiyo huku taasisi ya kusimamia majanga ikisema mtoto huyo alijeruhiwa katika tukio hilo.

Aidha taasisi ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani (USGS),  tetemeko hilo la kipimo cha ukubwa wa tetemeko 5.8 lilipiga jana usiku kwenye eneo hilo kaskazini mashariki mwa mkoa wa Badakhshan.

Hata hivyo vyombo vya habari nchini humo  viliripoti kusikika kwa mtikisiko katika maeneo mengi ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Kabul.Mara kwa mara, Afghanistan hukumbwa na matetemeko ya ardhi, haswa katika eneo la milima la  Hindu Kush.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii