Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.
Tetemeko kubwa la ardhi lenye
ukubwa wa 7.4 limetokea katika Bahari ya Molucca kaskazini mwa Indonesia, karibu na kisiwa cha
Ternate, kulingana na Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani.
Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya
Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.
Hakuna taarifa za mara moja kuhusu majeruhi, lakini
mitetemeko midogo ya baadae yenye ukubwa hadi 5 imeripotiwa.
Mamlaka za Indonesia zimeitaka baadhi
ya miji, ikiwemo Ternate na Tidore, kujiandaa kwa uwezekano wa uokoaji wa
dharura, huku baadhi ya majengo yakiripotiwa kuharibika.
Tetemeko hilo lilitokea katika kina cha takribani kilomita 35 na
kitovu chake kikiwa karibu kilomita 120 kutoka Ternate.
Maafisa wa tahadhari ya tsunami wamesema mawimbi hatari yanaweza kutokea ndani ya umbali wa kilomita 1,000 kutoka eneo la tukio.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime