Mvua kubwa nchini Kenya yauwa watu 81

Mvua kubwa iliyosababisha mafuriko nchini Kenya imewaua watu wasiopungua 81 mwezi huu. Hayo ni kwa mujibu wa mamlaka za nchini humo huku mvua ikiendelea kunyesha sehemu nyingi za nchi.

Katika eneo la magharibi mwa nchi lililoathiriwa kwa kiasi kikubwa, wakazi walipambana kwenye maji ya mafuriko na kuhamishwa kwenye boti zilizojaa watu. Mafuriko ya ghafla yalifunika vijiji katika kaunti ya Kisumu, na kuharibu takriban ekari 3,000 za mashamba yaliyokuwa na mazao.

Zaidi ya familia 3,000 zimelazimika kuhama makwao katika jamii ya Nyakach, huku baadhi zikihifadhiwa katika vituo vinane vya uokoaji, huku maji yanayoongezeka kutoka Mto Mirui unaofurika yakiendelea kutishia eneo hilo. Mji mkuu wa Nairobi una idadi kubwa zaidi ya vifo kutokana na mafuriko hayo, ambapo watu 37 wameripotiwa kufa.

Maafisa wamewataka wakaazi kuhama vitongoji kadhaa vya makazi duni vilivyoko upande wa chini wa mto karibu na bwawa la Nairobi, wakionya kuhusu hatari ya mafuriko huku viwango vya maji vikiongezeka na kutishia kuvunja ukingo wa bwawa hilo. Idara ya hali ya hewa inasema mvua inatarajiwa kuendelea hadi Jumanne.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii