Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limemkamata Ibrahimu Kitundu (18) Mkazi wa Kata ya Ipuli kwa tuhuma za kufanya shambulio la aibu kwa kuingiza uume wake kwenye mdomo wa Mtoto na kumlazimisha aunyonye ambapo Mtoto huyo aliunyonya hadi akatapika ambapo Ibrahim amesema alifanya hivyo ili kutimiza masharti ya Mganga ya kuwa Staa wa Filamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema “Mkoa wa Tabora tuna tukio la shambulio la aibu ambalo lilitokea March 22, 2026 majira ya saa sita mchana mtaa wa Nyerere Manispaa na Mkoa wa Tabora, alifanyiwa shambulio la aibu kwa kunyonyeshwa sehemu za siri na Ibrahimu Kitundu (18) Mnyaturu na Mkazi wa Ipuli”
“Siku hiyo Mtuhumiwa alimchukua Mhanga na kutoka nae nyumbani kwao na kumpeleka kwenye kibanda cha kurushia nyimbo za filamu kilichopo mtaani kwao kisha akamdanganya na kumuwekea sehemu zake za siri mdomoni na kumtaka azinyonye, Mhanga alifanya kama alivyoelekezwa na baadaye alimuacha”
“Walivyomuona akiwa na Mtoto huyo walimfuatilia na kumkuta Mhanga akiwa kwenye kibanda hicho huku akiwa anatapika, katika mahojiano Mtuhumiwa amekiri kufanya kitendo hicho na anaeleza kuwa alishawishiwa na Msanii mwenzake Mwanamke kwenye kikundi cha kuigiza kinachoitwa Nyanyembe Film ili kutimiza masharti ya Mganga ambaye aliwataka kupaka dawa na baadaye wakutane na kimapenzi na kisha kwenda kumnyonyesha Mtoto wa kiume na waliahidiwa watapata mafanikio kwenye kazi zao endapo wakifanya hivyo”
“Mtuhumiwa anashikiliwa kituo cha polisi na chanzo cha tukio ni imani za kishirikina na hatua nyingine za kisheria zinaendelea kuchukuliwa”
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime