Jeshi la Ulinzi la Mapinduzi la Iran (IRGC) limetoa onyo kali kwamba litachukua hatua za kulipiza kisasi iwapo sekta ya umeme ya nchi hiyo itashambuliwa.
Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, jeshi hilo limesema kuwa shambulizi lolote dhidi ya miundombinu ya umeme ya Iran litajibiwa kwa kushambulia vituo vya umeme vya Israel pamoja na vituo vinavyosambaza umeme kwa kambi za kijeshi za Marekani katika nchi za eneo la Mashariki ya Kati.
Taarifa hiyo imekuja wakati mvutano kati ya Iran, Israel na Marekani ukiendelea kuongezeka kufuatia vitisho vya mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Iran.
Iran imesisitiza kuwa itajibu shambulizi kwa hatua inayolingana na shambulizi hilo, hasa katika miundombinu ya umeme na nishati katika eneo lote la Mashariki ya Kati.
Hata hivyo tayari mvutano huo umechangia hofu ya kupanda kwa bei ya nishati na kuhatarisha usalama wa miundombinu muhimu kama vituo vya umeme, mafuta na maji katika nchi mbalimbali za eneo hilo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime