Maelfu ya waombolezaji siku ya Jumatano walikusanyika jijini Tehran nchini Iran kumwomboleza mkuu wa jeshi la maji la nchi hiyo Alireza Tangsiri, siku moja baada ya mazishi yake.
Waombolezaji walipeperusha bendera za Iran na mabango, wakitamka kifo kwa Marekani na Israeli.
Mkuu wa kikosi hicho cha majini, aliuawa wiki iliyopita kabla ya serikali ya Iran kutthibitisha kifo chake siku ya Jumatatu.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema Tangsiri alihusika pakubwa katika operesheni za Iran kuzuia safari za meli katika mlango wa Bahari wa Hormuz.
Mashambulizi ya Israeli, yalimuua pia kiongozi wa usalama wa taifa la Iran Behnam Rezaei.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime