DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JAMII NA WAZAZI KUSHIRIKI MALEZI YA WATOTO KIKAMILIFU

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa jamii na wazazi kushiriki kikamilifu katika malezi na ulinzi wa watoto, ili kuzuia ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani. 

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto anayeishi na kufanya kazi mtaani, yatakayofanyika Aprili 12, 2026 Jijini Dar Es Salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Malezi na Ulinzi wa Mtoto, Wajibu wetu Sote”. 

Amesema ushiriki wa pamoja ni muhimu ili kuhakikisha watoto wanakua katika mazingira salama na yenye maadili mema huku akisisitiza jukumu la malezi si la wazazi pekee, bali ni la jamii nzima. 

Aidha, Waziri Gwajima ameeleza kuwa changamoto kama umasikini, migogoro ya kifamilia, na ukatili dhidi ya watoto zimekuwa zikichangia watoto wengi kukimbilia mitaani. 

Ameibainisha pia mafanikio ya juhudi za Serikali katika kuwaokoa watoto wa mitaani kuwa zaidi ya watoto 5,000 wameunganishwa na familia zao tangu kuanza kwa kampeni ya kuwaokoa watoto wa mitaani mwaka 2025. 

Vilevile, Serikali imeanzisha mifumo mbalimbali, ikiwemo madawati ya ustawi wa jamii katika vituo vya usafiri na makao ya watoto, ili kuhakikisha watoto waliookolewa wanapata huduma muhimu kama elimu, afya, na malezi bora. 

Waziri Gwajima ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanapata malezi bora. 

Waziri Gwajima ametumia nafasi hiyo pia kuwashukuru wadau wote wanaoshirikiana na Serikali katika kuhakikisha malezi ya watoto yanaimarishwa hususani shirika  SoS Village na Railway Children. 

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote katika kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani, Amesema kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na halmashauri, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na jamii, kuhakikisha watoto hao waliokolewa wanarejeshwa katika familia 

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii