Wadau Waendelea Kutoa Maoni kwa Tume ya Uvunjifu wa Amani

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 27, 2026 imekutana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, kwa lengo la kupata maoni na ushauri wake kuhusu namna ya kuimarisha amani nchini.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Lake Tanganyika ndani ya Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam, ambapo pande hizo zimejadili chanzo cha matukio hayo, athari zake kwa wananchi, mali na miundombinu, pamoja na mapendekezo ya hatua za kuzuia yasijirudie.

Hivi karibuni, Tume iliongezewa muda wa siku 42 kuanzia Februari 20, 2026 ili kukamilisha kazi yake na kuwasilisha ripoti ifikapo au kabla ya Aprili 3, 2026.

Aidha kwa sasa, Tume inaendelea kukutana na wadau mbalimbali, wakiwemo waathirika, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutafuta suluhu ya kudumu na kuimarisha utulivu wa taifa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii