Ripoti zinaeleza kuwa idadi ya vifo vilivyotokana na vurugu zilizozuka mwishoni mwa juma nchini Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi mkuu wa Iran, imefikia watu 25 kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP ambapo aandamano yalizuka katika midhaa kadhaa mikubwa ya Pakistan, ikiwemo mji wa kusini wa Karachi, ambako baadhi ya waandamani walijaribu kuvamia majengo ya balozi za Marekani.
Mwandishi wa AFP alishuhudia mamia ya waandamanaji wanaounga mkono Iran wakijaribu kuingia katika ubalozi wa Marekani na hivyo kuchochea makabiliano na polisi. Mamlaka zimetangaza marufuku ya kutotoka nje usiku hadi Jumatano katika miji ya Gilgit na Skardu ambako kumesambazwa wanajehsi.
Maandamano hayo pia yalifanyika katika mitaa ya mji mkuu wa Islamabad ambako watu wawili wameuawa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime