Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Oman umetembelea Mkoa wa Pwani kwa lengo la kujionea shughuli za viwanda na biashara, na kuangazia fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na Oman katika sekta mbalimbali.
Ujumbe huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Mkoa wa Al Wusta na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman Dk. Salem Al-Junaibi.
Wafanyabiashara hao pia walitembelea Eneo la Viwanda la Kamaka na kuona maendeleo ya miundombinu pamoja na jitihada za Serikali za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Kesho, Septemba 8 mwaka huu ujumbe huo utatembelea makao makuu ya TCCIA na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya TCCIA ya Tanzania na Oman, na baadaye kushirki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji utakaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ukiwahusisha washiriki kutoka sekta ya umma na binafsi.