Kilimo, mifuko na Miundombinu kipaumbele cha Samia Mbeya

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapiduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuwekeza kwenye sekta za kilimo, mifugo na miundombinu ili kuinua maisha ya wananchi wa Mbeya na taifa kwa ujumla.

Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Mbalizi, Septemba 4 mwaka huu Samia amesema zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa eneo hilo ni wakulima, hivyo serikali imejipanga kuhakikisha wanapata pembejeo kwa ruzuku, huduma za ugani na masoko yenye uhakika.

“Tuliwasikia kilio chenu cha mbolea tangu 2022. Leo hii mbolea ya ruzuku inapatikana nchi nzima, na tumeboresha zaidi kwa kuweka mbolea mahsusi kwa kila zao. Lengo ni Tanzania kujilisha na kuuza ziada,” amesema.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali inakamilisha machinjio ya kisasa Utengule yatakayokuza thamani ya nyama na mifugo. Pia, ameahidi kukamilisha barabara na madaraja yote yaliyopo kwenye mpango wa CCM ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii