Devotha Minja aahidi kuboresha huduma za kijamii Kongwa

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja ameahidi kuwa Serikali ya chama itaboresha huduma za kijamii endapo wananchi watakipa dhamana ya kushika dola.


Devotta ameyasema hayo Septemba 4 mwaka huu wakati aliposimama kuwasalimia wananchi wengi wakiwa vijana waliokuwa eneo la Neto wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma.

Baada ya kusalimiana na vijana hao aliwaeleza dhamira ya chama hicho kusala dola kuunda Serikali ili kuwaletea maisha bora wananchi.

Baada ya maelezo hayo aliwapa vijana hao fursa ya kueleza changamoto wanazokumbana nazo, ambapo walisema maji safi na salama, barabara na vyoo ni kero kubwa kwenye maeneo yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii