Fahamu umri mrefu wa watu wa zamani na tofauti ya kizazi cha sasa

Watu wa zamani waliishi maisha yenye nidhamu ,mazoea ya kiafya na mshikamano wa kijamii ambao uliwasaidia kufikia umri mrefu kwa tofauti kubwa na kizazi cha sasa. Sababu kuu zinaweza kuelezea hali hii nikama ifuatavyo.

1: Mazoezi ya kimwili: Wazee wa kale walitegemea nguvu zao za mwili kwa shughuli za kila siku.

Walitembea umbali mrefu kwenda mashambani ,sokoni au kutafuta maji.

mfano halisi,katika jamii nyingi za kiafrika ,watoto na wazee walitembea kilomita nyingi kila siku wakienda shule au shambani bila usafiri wa kisasa kinyume chake,kizazi cha sasa kinatumia magari,pikipiki hata kwa umbali mfupi ,jambo linalopunguza uwezo wa mwili kufanya mazoezi.

2: Lishe ya Asili: Chakula cha watu wa zamani kilitokana zaidi na mazao ya shamba ,mboga mbichi na nyama zilizopikwa kwa njia rahisi kama kubanika au kuchoma.

 Kwamfano,jamii za wamasai walijulikana kwa kula nyama safi na maziwa mabichi bila kemikali:

vyakula hivi vilikuwa na viritubisho vya asili tofauti na vyakula vya sasa kama soda ,chips na vyakula vya mikate vinavyotengenezwa kwa kemikali nyingi.

Hii ndiyo sababu magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu yalikuwa nadra sana kusikika katika jamii za zamani.

3: Nidhamu ya Maisha: watu wazamani waliheshimu mila na desturi zilizoweka nidhamu . Kwa mfano kijana hangeweza kula chakula bila wazee kuridhia na hangeweza kufanya uamuzi mkubwa bila ushauri wa familia.

Nidhamu hii iliwasaidia kujenga tabia za heshima na mshikamano .kizazi cha sasa ,kutokana na utandawazi na mitandao ya kijamii,kinaiga mitindo ya maisha ya kigeni ambayo maranyingi inaleta uharibifu wa maadili na Afya.

4: Afya ya akili na Maisha ya kiroho: Kizazi cha zamani kilihusisha maisha yao na imani kwa Mungu na mshikamano wa kifamilia: kwa mfano,Familia nzima ilikusanyika jioni kuomba au kusimuliwa hadithi za kifamilia,jambo lililojenga mshikamano na kuondoa msongo wa mawazo .

Kwa sasa,familia nyingi zimegawanyika kila mtu anashughulika na simu janja au televisheni hali inayoongeza upweke, na matatizo ya afya ya akili . Shirika la Afya Duniani (WHO) limebaini ongezeko kubwa la msongo wa mawazo na unyongovu miongoni mwa vijana kutokana na mtindo huu wa maisha ya kisasa.

Kwaujumla,Umri mrefu wa watu wa zamani ulitokana na mchanganyiko wa mazoezi ya mwili,lishe bora,nidhamu ya maisha na mshikamano wa kiroho.Kizazi cha sasa kina mengi ya kujifunza kutoka urithi huu ili kuboresha afya na kuongeza matarajio ya maisha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii