Aliyemshitaki Mpina agoma kujivua uwanachama ACT

ALIYEDAIWA kufutwa uwanachama katika Chama cha ACT Wazalendo, Monalisa Ndala amekataa tamko la chama chake kumvua uwanachama, akidai yeye bado ni mwanachama halali wa chama hicho kwani barua hiyo haijatumwa kihalali na ni ukiukaji wa haki na demokrasia.

Amemtaka pia Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu kuikanusha barua hiyo ndani ya siku mbili kwani inakidhalilisha chama, akisisitiza uhalali wake ndani ya chama hicho na kuwa alichokifanya ni kwa lengo la kupigania mustakabali wa chama chake. Monalisa alieleza hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari akifafanua juu ya barua hiyo iliyotolewa na chama chake ya kumvua uanachama wake.

Alisema barua hiyo aliipata kwa kuchelewa na kutoka katika namba ngeni ambayo hakuitambua na barua hiyo imetoka katika kanda ambayo yeye si mwanachama wake.  “Mimi ni mwanachama hai na kiongozi wa chama wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenezi wa Jimbo la Kibamba,” alisisitiza. Alisema aliwahi kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na alipita kwa asilimia 72, lakini aliitwa na mwanasheria mkuu wa chama hicho na kuelezwa amekiuka utaratibu na kanuni kwani yeye ni mwanachama na mwenezi wa Dar es Salaam. “Mimi sijapoteza uanachama wangu na nitaupigania,” alisema.

Alisema lengo la chama ni kubadilisha ajenda ya mgombea urais wao, Luhaga Mpina kwani viongozi hawataki kukubali namna wamekigharimu chama kwani wanakwenda kukosa mgombea wa urais na wawajibike.

Monalisa hivi karibu aliandika barua kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa akilalamika uamuzi wa chama hicho wa kumsimamisha Mpina kugombea urais kuwa umekiuka sheria na kanuni za uteuzi wa mgombea huyo. Katika kujua msimamo wa chama juu ya yaliyozungumzwa na Monalisa katika mkutano huo,na vyombo vya habari ilifanya jitihada za kumtafuta Shaibu na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Shangwe

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii