KAMPUNI ya ORYX GAS kwa kushirikiana na meneja mkuu wa
mauzo na masoko tanzania bara na
visiwani Shaban Sungi wameendelea kujidhatiti na kuwafikia wananchi wa Buhongwa
wilaya ya nyamagana mkoani Mwanza kwa kutoa hamasa katika matumizi ya nishati
safi ya kupikia.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kueendeleza kampeni ya gesi sungi amesema kuwa matumizi ya nishati chafu ya kupikia imekuwa ikisababisha vifo hasa kwa kinamama
Shabani amesema kuwa tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya gas yente imekuwa na mwitikio mkubwa kwa wananchi kutokana na elimu wanayoitoa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kwa upande wake katibu tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Jemes Salala ameipongeza kampuni ya ORYX kwa kutambua uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala kwa kuongeza chachu kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Nao baadhi ya washindi wa zawadi mbalimbali kutoka kwenye
kampuni ya ORYX GAS wametoa pongezi zao za dhati kwa hamasa na elimu wanayoipata juu ya matumizi ya nishati
safi ya kupikia.