Profesa Palamagamba Kabudi na Spika Dk Tulia Ackson wamebainisha sababu za wananchi kumuamini Rais Samia Suluhu Hassan na kumpa kura za kishindo katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza na umati wa wananchi kwenye mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tandale, katika mji wa Tukuyu Wilaya ya Rungwa, Profesa Kabudi alisema Rais Samia anashahili kuchaguliwa kwasabu ameongeza kasi ya kuepeleka maendeleo vijijini.
Alisema kwa kupeleka huduma za kijamii kama elimu, afya, nishati ya umeme na huduma ya maji vijiji vimepata maendeleo hivyo kutimiza azima ya Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere ya kupeleka maendeleo vijijini.
Alisema pia ni kutokana na kuwa mgombea wa CCM, chama chanye uzoefu na uwezo wa kuongoza nchi na kuwaletea wananchi maendeleo.
Profesa Kabudi alisema kiongozi ambaye anaweza kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwani mpaka sasa ametoa ruzuku kwenye mbolea, mbegu na pembejeo nyingine.
Pia ameweza kusogeza huduma za afya kwa wananchi kwa kujenga vituo vya afya takribani 1,000, imarisha miundombinu ya barabara hususani maeneo ya vijijini, ameinua sekta ya utalii na kufikisha nishati ya umeme huku akiwa katika mchakato wa kuzalisha umeme kupitia jotoardhi.
Kwa upande wa Spika Dk Tulia ambaye pia ni mgombea wa Jimbo la Uyole alisema wananchi hususani wanaRungwe ni mashahidi ya miradi ya huduma za kijamii ambazo zimepelekwa katika maeneo yao.
“Wananchi tujitokeze kwanza kutafuta kula, kuzilinda lengo ni kuhakikisha wana Rungwe tunampa kura za heshima ili tuendelee kunufaika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi. Mheshimiwa mgombea wetu tunaenda kukuheshimisha.”