Kesi hiyo imepangwa leo Septemba 8 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali mbele ya Jaji Dunstan Ndunguru, huku upande wa Jamhuri ukitarajia kuwaita Mashahidi 30 kutoa ushahidi dhidi ya Lissu na kuwasilisha vielelezo 16.
Itakumbukwa awali kesi hiyo ilikuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na baada ya kukamilishwa kwa upelelezi ikahamishiwa rasmi katika Mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na hatua zaidi za kisheria.
Katika kesi hiyo ya uhaini Lissu anadaiwa Aprili 3 mwaka huu akiwa katika Mkutano wa hadhara Jijini Dar es salaam, alizungumza maneno yaliyotafsiriwa kuwa na nia ya kushawishi au kuchochea umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii