RUWASA kutekeleza mradi mkubwa wa maji Kikuku-Muleba

Zaidi ya wananchi 6,961 wameondokana na changamoto ya maji baada ya Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutekeleza mradi mkubwa wa maji ambao unavigusa vijiji vya Nsisha Kagoma na kikuku wilayani Muleba mkoani Kagera.

Hii ni moja ya mradi ambao umeleta furaha kwa wananchi wa kata ya Kikuku ambao wameshuhudia mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 ukiweka Jiwe la Msingi katika mradi huo.

Ashura Juma, mkazi wa Kagoma amesema kwa miaka mingi kata hiyo na vijiji vyake wamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji  hasa nyakati za Kiangazi ambapo watoto walipitia ukatili mkubwa Wa kingono na wazazi kuwachapa fimbo kutokana na kutumia muda mrefu  kutafuta maji

Zida Milanga mkazi wa Kikuku ameipongeza serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji katika vijijini vya pembezoni na kuondoa adha kwa wananchi ambao walikuwa wanatumia muda mrefu kufuata maji.

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Muleba, Paschale Kibangule amesema mradi huo umegharimu Sh milioni 650 na umefikia asilimia 89 , tayari wananchi wameanza kuunganisha maji majumbani  huku mradi huo ukitarajia kukamilika Oktoba 25 mwaka huu.

Amesma kazi zilizofanyika mpaka sasa ni  ujenzi wa tanki kubwa la maji ujazo wa Lita 150,000,ujenzi wa chanzo Cha Maji , mtandao wa mabomba Kilometa 14.7 ujenzi wa vituo 17 vya kuchotea maji, ujenzi wa ofisi za CBWSo,s

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu Ismail Ussi amelizishwa na utekelezaji wa mradi huo ambapo ametoa wito kwa wananchi kulinda vyanzo vya maji Ili Kusaidia kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha alitoa wito kwa wananchi kutofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji na kutoharibu miundombinu ya maji huku akiwahakikishia wananchi wa wilaya ya Muleba kuwa serikali utaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa kila Kijiji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii