Rais Ramaphosa Akataa Rapa AKA Kufanyiwa Mazishi ya Kitaifa

Vyombo vya Habari vya AfrikaKusini vimeripoti kuwa Gavana wa Serikali ya Gauteng Panyaza Lesufi, alimwandikia Rais #Ramaphosa ombi la Msanii huyo kuzikwa kama Mtu mwenye mchango mkubwa kwa jamii na hivyo apewe heshima ya Kitaifa


Gavana Panyaza hakuomba fedha za Serikali zitumike kwa ajili ya mazishi, bali Jeneza tu la Rapa huyo lifunikwe kwa Bendera ya Taifa pamoja na muda mchache wa Bendera kupepea nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo


Rapa #KiernanForbes 'AKA' aliuawa kwa kupigwa Risasi nje ya Mgahawa Februari 10, ikiwa ni muda mchache akijiandaa kusherehekea Siku yake ya Kuzaliwa pamoja na rafiki zake. #AKA atazikwa Jumamosi Februari 17, 2023


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii