Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko amesema uhusiano na Morocco ni "imara zaidi kuliko hisia" siku chache baada ya vurugu zilizozuka wakati mataifa hayo yalipokabiliana katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Akizungumza mjini Rabat jana Jumatatu kwenye mkutano wa kamisheni ya pamoja ya Senegal na Morocco, Sonko amesema ziara yake haimaanishi kutuliza hali lakini ililenga kuthibitisha uhusiano baina ya mataifa hayo.
Amesema kwenye mkutano ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Morocco, Aziz Akhannouch kwamba yaliyoshuhudiwa yanapaswa kuchukuliwa kama yaliyotokana na hisia zilizochochewa na mapenzi na sio kwa sababu za kisiasa ama kitamaduni.
Mechi ya fainali ya AFCON kati ya Morocco na Senegal mjini Rabatt ilivurugika baada ya wachezaji wa Senegal kutoka nje ya uwanja kufuatia penati yenye utata waliyopewa Morocco.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime