Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, ametangaza kuwa mipango ijayo ya nchi yake ya kuongeza hazina ya silaha za nyuklia itawekwa wazi wakati wa mkutano mkuu wa chama tawala utakaofanyika wiki kadhaa zinazokuja.
Shirika la Habari la Korea Kaskazini, KNCA, limemnukuu Kim akisema mkutano huo mkuu utafafanua mipango na hatua zinazofuata kwa nchi hiyo katika kuimarisha nguvu zake za nyuklia kama kinga dhidi ya uvamizi kutoka nje.
Kim amekaririwa akiyasema hayo wakati aliposhuhudiajaribio la pili ndani ya mwezi Januari la makombora ya masafa lililofanywa hapo jana jaribio hilo lilihusisha kufyetuliwa makombora manne yaliyoanguka baharini umbali wa kilometa 359.
Kwa miomgo kadhaa sasa mradi wa nyuklia na makombora ya masafa waKorea Kaskazini umekuwa chanzo cha misuguanona nchi za maghribi hususani Marekani ambayo imeiwekea nchi hiyo vikwazo vikali vya kiuchumi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime