Saudi Yasema Haitaruhusu Ardhi Yake Kutumika Kushambulia Iran

Saudi Arabia imesema haitoruhusu anga wala ardhi yake kutumika kwa oparesheni yoyote ya kijeshi kuishambulia Iran.

Saudi Arabia imesisitiza kuwa haitaruhusu ardhi yake kutumika kutekeleza shambulizi lolote la kijeshi dhidi ya Iran, kwa mujibu wa mazungumzo ya simu kati ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian.

Taarifa hiyo imeripotiwa na Shirika la Habari la Saudi Arabia (SPA), likinukuu sehemu ya mazungumzo hayo yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa SPA, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambaye ni mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, amemhakikishia Rais Pezeshkian kuwa utawala wa Riyadh unaheshimu uhuru, mamlaka na mipaka ya Iran, na kusisitiza kuwa Saudi Arabia haina nia ya kushiriki au kuruhusu matumizi ya ardhi yake kwa mashambulizi dhidi ya Tehran.

Kauli hiyo inakuja katika kipindi cha mvutano unaoongezeka katika eneo hilo, huku kukiwa na wasiwasi kwamba Marekani huenda ikachukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran, baada ya kuituhumu serikali ya Tehran kuhusika na mauaji pamoja na ukandamizaji wa waandamanaji wa umma mapema mwezi huu.

Mazungumzo hayo yanaonekana kuwa sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano na kulinda utulivu wa kikanda.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii