Aliyekuwa Kipa wa Taifa Stars na Yanga, Peter Manyika Amefariki

Aliyekuwa kipa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Yanga SC, Peter Manyika amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya St. Monica jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa familia na vyanzo vya karibu vimesema kuwa chanzo cha kifo cha Manyika ni kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa akipatiwa matibabu kabla ya umauti kumkuta.

Hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala  iliyopo jijini Dar es Salaam kwaajili ya taratibu zaidi za kifamilia na maandalizi ya mazishi yatakayotangazwa baadaye.

Aidha Peter Manyika atakumbukwa kama mmoja wa makipa waliolitumikia kwa uaminifu soka la Tanzania akiwa kama sehemu ya kikosi cha Taifa Stars pamoja na Klabu ya Yanga SC katika nyakati tofauti za taaluma yake na uzoefu wake, nidhamu na mchango wake ulibaki kuwa sehemu ya kumbukumbu muhimu katika historia ya soka la nchi.

Hata hivyo Kifo cha Manyika kimepokelewa kwa huzuni kubwa miongoni mwa wanafamilia, wadau wa michezo, wachezaji wa zamani na mashabiki wa soka nchini ambao wameendelea kutoa salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii