Tume Huru ya Uchunguzi wa vurugu za Oktoba 29 nchini Tanzania imezuia wanahabari kushiriki katika mahojiano yanayoendelea kati ya tume hiyo na waathirika wa matukio hayo ikieleza kuwa uchapishaji wa taarifa zao binafsi unachochea msongo wa mawazo kwa wahanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume, uamuzi huo umechukuliwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa waathirika kwamba maelezo yao binafsi yamekuwa yakisambazwa mitandaoni bila ridhaa yao, jambo linalokiuka faragha na kuathiri ustawi wao wa kisaikolojia.
Tume imesisitiza kuwa lengo la hatua hiyo si kuwanyima waandishi habari taarifa, bali kulinda haki na usalama wa waathirika wakati wa mchakato wa uchunguzi unaoendelea.
Aidha imetoa wito kwa vyombo vya habari kuzingatia maadili ya uandishi kwa kuheshimu faragha za wahanga huku ikiahidi kuendelea kutoa taarifa rasmi kwa umma bila kuhatarisha maslahi ya waathirika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime