Klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani Freiburg usiku wa kuamkia leo imeendeleza msururu wake wa kutofungwa katika mechi za Ligi ya Ulaya kwa kuilaza Maccabi Tel Aviv 1-0 na kujikatia tiketi ya hatua ya 16 bora.
Christian Günter ndiye aliyefunga bao hilo la ushindi kunako dakika ya 82 kwengineko azma ya VfB Stuttgart ya kufuzu moja kwa moja kwenye hatua hiyo ya mtoano ya mashindano hayo ya Ulaya imeingia doa baada ya kufungwa 2-0 na AS Roma ya Italia.
Kwa kushindwa huko Stuttgart sasa wanaishikilia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ya Ulaya.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime