Ouahbi Aanza Kazi Kuijenga Upya Morocco

Royal Moroccan Football Federation limemtangaza Mohamed Ouahbi kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa ya wanaume ya Morocco national football team maarufu kama The Atlas Lions, akichukua nafasi ya Walid Regragui ambaye alitangaza kujiuzulu Machi 5, 2026.

Baada ya uteuzi huo, Ouahbi amepewa jukumu la kuhakikisha Morocco inaendelea kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, hususan FIFA World Cup 2026.

Katika michuano hiyo, Morocco imepangwa Kundi C pamoja na Brazil national football team, Scotland national football team na Haiti national football team.

Hata hivyo kocha Ouahbi pia anatarajiwa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na Morocco katika FIFA World Cup 2022, ambapo timu hiyo iliweka historia kwa kufika hatua ya nusu fainali, na sasa anapewa dhamana ya kuhakikisha kikosi hicho kinaendelea kung’ara katika soka la kimataifa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii