Rodrygo Nje Miezi 7–10, Aikosa Kombe la Dunia 2026

Mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil national football team, Rodrygo, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi saba hadi kumi kufuatia jeraha kubwa, hali itakayomfanya kuukosa msimu mzima wa 2026 pamoja na michuano ya FIFA World Cup 2026 itakayoanza mwezi Juni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rodrygo ameweka wazi maumivu na huzuni aliyonayo baada ya ndoto yake ya kushiriki Kombe la Dunia kufifia kutokana na jeraha hilo.

Amesema siku aliyopata taarifa ya ukubwa wa tatizo lake ilikuwa miongoni mwa siku ngumu zaidi katika maisha na taaluma yake ya soka.

“Bila hata kuelewa, nakuamini… Labda maisha yamekuwa magumu kwangu hivi karibuni. Kikwazo kikubwa kimejitokeza katika maisha na kazi yangu, kinachonizuia kufanya ninachokipenda zaidi kwa muda,” aliandika nyota huyo, akionesha imani yake kwa Mungu licha ya changamoto hiyo.

Rodrygo ameongeza kuwa licha ya kukosa msimu uliosalia na kushindwa kuitumikia Brazil katika Kombe la Dunia, ataendelea kuwa imara na kurejea akiwa na nguvu zaidi. Amewashukuru familia, mashabiki na wote waliomtumia ujumbe wa faraja, akisisitiza kuwa huu si mwisho wake bali ni “kwa heri ya muda mfupi.”

Hata hivyo jeraha hilo ni pigo kubwa kwa Real Madrid katika mipango yao ya msimu ujao, sambamba na Brazil waliomtegemea kama mhimili muhimu kuelekea Kombe la Dunia 2026.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii