Mamia ya raia kwenye mji wa Tigray nchini Ethiopia, wameanza kuondoka kwenye maeneo yao kutokana na kuongezeka kwa hofu ya kuzuka kwa mapigano mapya kati ya vikosi vya Serikali na wapiganaji wenye silaha wa Tigray.
Katika jiji kuu la Tigray, Mekelle, vijana wengi wamekuwa wakionekana usiku wakiwa na mabegi na mizigo yao kutafuta usafiri wa basi kuelekea Addis Ababa.
Wenyeji wamekuwa wakilalamikia uhaba wa bidhaa muhimu ikiwemo mafuta ambayo yamekuwa yakiuzwaa kwa magendo na kwa bei ya juu.
Waziri mkuu Abiy Ahmed amenukuliwa akitoa hakikisho kuwa hana nia ya vita ,hata hivyo ,vikosi vya serikaki na Tigray vimekuwa vikijiandaa katika mpaka wa kaskazini mwa Ethiopia, pande zote zikilaumiana kwa uhasama unaoendelea kuonekana.
Amanuel Assefa ambaye ni kamanda wa pili katika uongozi wa wapiganaji wa Tigray, amesema majeshi ya serikali yamekuwa yakizunguka eneo hilo, haya yakijiri miaka minne baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani wa Pretoria uliomaliza vita vilivyodumu kwa karibu miaka miwili huko Tigray.