Mabalozi wa NATO kukutana na wenzao wa Ghuba

Mabalozi wa jumuiya ya kujihami ya NATO watakutana na wenzao wa nchi za Ghuba kuijadili hali ya vita vinavyoendelea nchini Iran.

Mabalozi kutoka nchi 32 wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO wanapanga kukutana na wawakilishi wa eneo la Ghuba wiki ijayo kujadili vita vya Iran na mvutano wa kikanda ambapo hayo ni kwa mujibu wa wanadiplomasia watatu wa Ulaya walipozungumza na shirika la habari la Reuters.

Hata hivyo wanadiplomasia hao walisema mabalozi hao wanatarajiwa kufanya majadiliano na wenzao kutoka Bahrain, Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii