Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na viongozi wa kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda duniani za G7 Jumatano kujadili mgogoro wa Iran na kupanda kwa bei za nishati.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na viongozi wa kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda duniani za G7 leo Jumatano kujadili mgogoro wa Iran na kupanda kwa bei za nishati. Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya rais wa Ufaransa.
Mazungumzo hayo yanakuja huku serikali za mataifa ya G7 zikizingatia jinsi ya kukabiliana na ongezeko kubwa la bei za mafuta lililosababishwa na vita kati ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran.
Mawaziri wa nishati wa G7 walisita kukubaliana kuhusu kutolewa kwa akiba ya mafuta ya kimkakati siku ya Jumanne na badala yake waliliomba shirika la nishati la kimataifa kutathmini hali hiyo kabla ya kuchukua hatua.
Ufaransa ndiyo mwenyekiti wa sasa wa muungano wa G7 unaozajumuisha pia Marekani, Kanada, Japan, Italia, Uingereza na Ujerumani.