Wanamgambo washambulia kituo cha jeshi Burkina Faso

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa itikadi kali wameshambulia hapo jana kituo cha wanajeshi katika mji wa kaskazini mwa Burkina Faso wa Nare.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa makumi ya watu wameuawa. Huu ni mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni ya makundi ya kigaidi ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 10 katika muda wa siku nne.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayoongozwa na utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2022, imekuwa ikikumbwa na vurugu za mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wenye mafungamano ya muda mrefu na  makundi ya kigaidi  ya Al-Qaeda au lile linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii