Zelensky asaka mifumo zaidi ya ulinzi wa anga

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amewarai washirika wake kumpatia mifumo zaidi ya ulinzi wa anga kujikinga na mashambulizi ya Urusi ambayo amesema yameongeza madhila kwa umma wa Ukraine msimu huu wa baridi.

Zelensky ametoa mwito huo alipowasili kwenye mji mkuu wa Lithuania, Vilnius, kushiriki kumbukumbu ya vuguvugu la umma lililotokea nchini Poland na Lithuania mwaka 1863 dhidi ya utawala wa Urusi ya zamani.

Amesema wiki hii pekee, Urusi imefanya mashambulizi zaidi ya 1,700 ya droni, mabomu 1,380 na makombora 69 nchini Ukraine. Amesisitiza hali hiyo ndiyo inafanya kuwa muhimu kwa serikali yake kuomba msaada zaidi wa ulinzi wa anga.

Amearifu kuwa tayari anafanya mazungumzo na Marekani na Ulaya kuhakikisha wanapata ulinzi madhubuti wa anga dhidi ya hujuma za Urusi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii