DRC Yapiga Marufuku Uandikishaji Mpya wa Wafungwa Gereza la Makala

Waziri wa Nchi anayehusika na Sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Guillaume Ngefa, amepiga marufuku kwa muda uandikishaji wowote mpya wa wafungwa katika Gereza la Makala jijini Kinshasa.

Hatua hiyo iliyoanza kutekelezwa Februari 14, inalenga kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliosababisha vifo vya wafungwa watano gerezani hapo.

Kwa mujibu wa waraka wa Waziri huyo, maafisa wa magereza, mamlaka za afya pamoja na huduma zote muhimu wameelekezwa kuhakikisha utekelezaji mkali wa hatua hizo na ufuatiliaji wa karibu wa hali ya afya gerezani.

Mratibu wake, Emmanuel Cole, amesema kuwa kwa sasa kuna takribani wafungwa 11,404 katika gereza hilo lenye uwezo wa kuchukua wafungwa 1,500 pekee, hali inayoonyesha msongamano mkubwa unaochangia hatari ya milipuko ya magonjwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii