Jackie Chan Ajiandalia Wimbo wa Mazishi

Imeelezwa kuwa muigizaji maarufu wa filamu duniani Jackie Chan, tayari ameandaa wimbo maalum wa kuchezwa siku atakayofariki pamoja na siku ya mazishi yake. Taarifa hizo zimedaiwa kujitokeza baada ya staa huyo kuhudhuria tukio la kwanza la filamu yake lililofanyika Disemba 28, 2025.

Aidha katika tukio hilo Jackie Chan anaripotiwa kuwa aliwaomba watu wake wa karibu na timu yake ya kazi kuandaa wimbo huo mapema huku akisisitiza kuwa uachiwe rasmi siku atakapoaga dunia. Hatua hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa filamu duniani.

Hata hivyo Jackie Chan ni mmoja wa waigizaji walioweka historia kubwa katika tasnia ya filamu, akiwa ameigiza katika filamu zaidi ya 95 ndani ya maisha yake ya uigizaji na kutambulika kwa michango yake katika filamu za mapigano, vichekesho na burudani kwa ujumla.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii