Jimmy Lai bilionea aliyekuwa akimiliki yombo vya habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa China ametiwa hatiani kwenye kesi ya aina yake kuhusiana na usalama wa taifa hukumu ambayo inampeleka jela maisha.
Majaji wa Mahakama ya Hong Kong waliamua jioni ya Disemba 15 mwaka huu kwamba Lai mwenye umri wa miaka 78 ana hatia ya kula njama na wenzake kwa kushirikiana na wageni kuhatarisha usalama wa taifa na kuchapisha makala za uchochezi.
Aidha Lai aliyekamatwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 2020 chini ya sheria kali ya usalama iliyoanzishwa na utawala wa Beijing kwa na makosa ya aina hiyo.
Hata hivyo kwa muda wa miaka mitano mpiganiaji huyo wa demokrasia amekuwa kizuizini sehemu kubwa zaidi akiwa ametengwa, huku familia yake ikisema afya yake imekuwa ikidorora kwa haraka.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime