Rais wa zamani wa Korea Kusini (2022–2025), Yoon Suk Yeol, ameomba radhi kufuatia taharuki na mjadala ulioibuka baada ya uamuzi wake wa kutangaza Sheria ya Kijeshi mwishoni mwa mwaka 2024.
Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya Mahakama kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuongoza uasi.
Ingawa pamoja na hukumu hiyo, Yoon amesisitiza kuwa hatua yake ilikuwa na lengo la kuilinda na kuiokoa nchi dhidi ya kile alichodai kuwa hatari kwa utawala wa taifa.
Amesema ni vigumu kukubaliana na hoja kwamba kupelekwa kwa wanajeshi katika Bunge la Taifa kulikuwa sawa na kitendo cha uasi.
Aidha Mahakama imeeleza kuwa msingi wa kesi hiyo ulikuwa ni uamuzi wa kupeleka wanajeshi katika Bunge la Kitaifa wakati wa utekelezaji wa Sheria ya Kijeshi.
Hivyo basi kwa mujibu wa uamuzi huo, hatua hiyo ililenga kupooza na kuzuia shughuli za chombo hicho cha kikatiba.
Hata hivyo kesi hiyo imeibua mjadala mpana wa kisiasa na kikatiba kuhusu matumizi ya mamlaka ya kijeshi katika mfumo wa kidemokrasia nchini Korea Kusini.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime