Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, leo Februari 20, 2026, amempokea ofisini kwake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Mhe. Deus Sangu, aliyewasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Sangu anatarajiwa kushiriki ufunguzi wa mafunzo ya udereva wa pikipiki na bajaji yatakayofanyika jijini Mwanza. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea vijana ujuzi wa vitendo ili waweze kujiajiri na kuboresha kipato chao.
Mafunzo hayo yanaandaliwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wakiwemo Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mwanza pamoja na taasisi ya kifedha ya CRDB.
Ziara ya Waziri huyo inalenga pia kuhimiza ajira stahiki na kuendeleza juhudi za Serikali katika kuwainua vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya ufundi na ujasiriamali.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili mchana ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @jacobmlay__ tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime