Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo Jumatatu Desemba 15, 2025, inatarajiwa kusikiliza maombi Na. 289778/2025 yaliyofunguliwa na Waziri wa zamani Geoffrey Mwambe dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO DSM).
Maombi hayo ambayo yamefunguliwa Mahakamani hapo na Mwambe kupitia Wakili wake Hekima Mwasipu, yanatarajiwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Gwantwa Mwankuga.
Taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro Desemba 12 mwaka huu, ilieleza kuwa Jeshi hilo linamshikilia Mwambe kwa tuhuma za jinai ambazo zinachunguzwa.
Jeshi la Polisi lilitibitisha kumshikilia Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Masasi usiku wa Desemba 07, 2025 eneo la Tegeta, Dar es Salaam.